Mchakato wa uandikishwaji wa watu katika daftari la kupiga kura.

Ikiwa zimebaki siku chache kabla ya upigaji wa kura katika uchaguzi wa serikali za mitaa 2019,Mhe.Selemani S.Jaffo(Mb) na waziri wa TAMISEMI ametoa rai kwa wananchi wote kutumia vizuri muda uliowekwa wa siku saba kuanzia tarehe8-14/10/2019 kuhakikisha wanajiandikisha kwenye orodha ya daftari la wapiga kura ili kupata haki yao ya msingi wa kushiriki kuwapigia kura wagombea wao.
Pia ameweza kueleza sababu za msingi ikiwepo ni kupata haki ya msingi kama raia wa Tanzania na licha kupata haki ya msingi vilevile ukijiandikisha utaweza kugombea nafasi za uongozi katika ngazi ya serikali za mitaa.