NANI NIMPE MOYO WANGU!!? 

Moyo ni kiungo maarufu sana unapunguzia swala la mapenzi. Kila kukicha moyo hutajwa na watu Zaidi pindi wanapozungumzia mahusiano ya kimapezni na sijajua nini sababu ya kuhusishwa moyo katika swala la mapenzi unaweza jiuliza katika hili labda moyo ni kiungo pekee kinachopatwa maumivu Zaidi katika mapenzi.zaidi ya mamia hufa kwa mshituko wa moyo() pindi habari ya ghafla inapowafikia .Wasanii pia ni watu wanaozungumzia moyo katika uandishi wao haswa wanapotunga nyimbo za mapenzi.Moyo umepewa thamani kubwa sana katika

mapenzi na sababu ya kutokea kwa swali nani nimpe moyo wangu!!!?

Hofu
Hofu imekuwa kigezo tosha la binadamu kutowaamini binadamu wenzao unapohusisha swala zima la mpaenzi.binadamu hupokea hofu kutokana na mazingira husika yanayowazunguka na Imani ya ndani katika vichwa vyao namanisha mazingira yanamsababishia hofu binadamu kwa kuona mambo yanavyoendelea. Imani ya ndani ni baada ya kujihusisha mojawapo katika mahusiano na kupata matokeo mbalimbali. Hofu hugawanyika uwanja mpana sana 

                 🔺Hofu ya usaliti na
          🔺Hofu ya udanganyifu:
          🔺Hofu ya kupata matokeo hasi



Njia za kumpata anayekufaa katika mahusiano...
Wengi wamekua wakiangalizia sababu au njia za kumpata anayekufaa katika mahusiano katika sekta mbalimbali na zimekuwepo sababu au njia nyingi za kumpata anayekufaa katika mahusiano , ila wacha nikupe njia mbili tu ambazo zitakujenga kimawazo kwenye kufanikisha kumpata mwenza wako:

#Kuangalia udhaifu wako
Udhaifu ni moja ya sababu au sifa ya binadamu kwa maana kila mtu kaumbwa na hulka yake na tabia ya kipekee katika kulipokea jambo au kulifanya jambo. Binadamu tuna tofautiana kidogo sana katika udhaifu unaojitokeza katika mahusiano. Angalia udhaifu wako ili kukuwezesha kumpata mwanamke au mwanaume ambaye mtaendana katika mahusiano yenu. Kubali una madhaifu kwa maana tumeumbwa na udhaifu na yakupasa kumchagua ambae atayajua madhaifu yako na kuyakubali katika hali tofauti. Mojawapo ya udhaifu ni hasira zisizo za maana na zenye maana, kupenda utawala katika mahusiano hili linajumuisha kupenda kusikilizwa upande mmoja tu wa mahusiano kama mwanamke basi ni mwanamke mwenye maamuzi au kama ni mwanaume basi ni mwanaume anayeweza kutoa maamuzi na kufatishwa bila kuangalia upande mwengine wa mahusiano.Tbia ya kutojali pia inahusishwa ni mojawapo ya madhaifu yanayopelekea ugomvi na malumbano katika mahusiano baina ya wawili.


#Kuangalia lifestyle yako:
Yaweza kuwa watu wengi huingia katika mapenzi bila kuangalia mtindo wa maisha(lifestyle) yao ili kuweza kupata mwanamke au mwanaume ambaye anayemfaa katika maisha yake. Kuwa na uhakika na mtindo wa maisha yako au pendekezo la mtindo wa maisha ya mwanaume au mwanamke unayemtaka.Kama wewe ni mwanamke au mwanaume unayependa ukimya na usiri jaribu kuchukua mwanaume au mwanamke ambaye utahisi anaweza akaendana na falsafa zako kwenye maisha. Usijaribu kuchukua ili mladi umechukua kwa mana thamani ya moyo ni kubwa sana hebu chukua mwenye uendano sawa na wewe.


NB:
Muhusishe Mungu katika utambuzi wa mwanamke au mwanaume bora wa maisha yako mana yeye ndo anayeijua hatima yako hata kabla ujatenda.


                                                                           ASANTE SANA