Mapenzi Ni Pesa ?
Mapenzi pesa ni swala amabalo limeteka vichwa vya habari
katika mahusiano ya wengi. Wengi hulalama ya kuwa hakuna mapenzi bila ya kuwa
na pesa wengine wakisema tafuta pesa mapenzi yatakuja. Ni jambo linalochanganya
wengi hata kwa wanaotoa ushauri wa mapenzi nao wamekua wahanga wa swala hili.
Ni kweli mapenzi pesa?
Pesa yaweza kuwa kichocheo mojawapo ya kulifurahia penzi
lenu kwa upande mmoja au mwengine. Mfano kuna vizawadi vya ghafla ambavyo
wapenzi wengi hupenda kufanyiana na mituko ya hapa hapa na pale. Ila ukweli wa
mambo unasema mapenzi yamegawanyika katika pande mbili mapenzi ya dhati na
yasiyo ya dhati.
Wengi ambao wana mapenzi ya dhati swala la pesa limekuwa likishika
nafasi ndogo sana(minor) kwa maana hata isipokuwepo waweza furahia na kudumisha
mapenzi yao katika ustadi wa hali ya juu.
o
#MAPENZI YASIYO YA DHATI:
Wengi huyapenda mapenzi ya kuigiza kiupande ambao utahisi
unamteka mwenza wako kiakili na kutambua kuwa unampenda ila la hasha! Huna ata
moja unalomuwazia Zaidi ya udanganyifu tu.Katika sekta hii pesa imekuwa ni
silaha tosha ya kudumu na mwenza wako
0 Comments